Tukio hili lilikuwa kiashiria cha wazi kuwa Qur’an ni kitovu cha mshikamano, upendo, na amani siyo tu miongoni mwa Waislamu, bali pia kwa jamii nzima ya kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Tanzania — Maelfu ya Wananchi, Waislamu kwa wasiokuwa Waislamu, walifurika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia Kongamano kubwa la Qur’an Tukufu lililofanyika kwa mafanikio makubwa na kwa hali ya kipekee isiyosahaulika.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wasomaji bingwa wa Qur’an Tukufu kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo mabingwa kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania.
Washiriki walionyesha umahiri wa hali ya juu katika usomaji wa Qur’an kwa Tajweed sahihi, sauti nzuri na za kuvutia, hali iliyogusa na kuamsha hisia za kiroho kwa maelfu ya waliohudhuria.
Tukio hilo lilikuwa kiashiria cha wazi kuwa Qur’an ni kitovu cha mshikamano, upendo, na amani siyo tu miongoni mwa Waislamu, bali pia kwa jamii nzima ya kitaifa na kimataifa.
Hili lilidhihirika wazi kupitia hali ya utulivu, maelewano, na mshikamano uliotawala Kongamano zima.
Qur’an ni nuru, ni mwanga unaoangaza mioyo yetu. Leo tumeona namna ilivyo kiungo cha umoja wetu.
Kwa hakika, nyoyo za Waumini ziliburudika kwa kusikiliza maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu yakisomwa kwa umahiri mkubwa.
Hali hiyo iliwaacha wengi na hisia za matumaini, furaha na hamasa ya kuimarisha imani yao na kuendeleza mshikamano wa kidini na kitaifa.
Kongamano hili ni ushahidi wa wazi kuwa Qur’an bado ina nafasi kubwa na ya kipekee katika maisha ya jamii ya Kitanzania, na kuwa chombo muhimu cha kuimarisha maadili, mshikamano, na amani ya kudumu.
Your Comment